Sisi UVIMA SACCOS ni nani?

UVIMA SACCOS HUONDOA UMASKINI NA KUBORESHA MAZINGIRA YETU

UVIMA ni kifupi cha maneno - Umoja wa VICOBA Marangu

Hiki ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo kilichoanzishwa tarehe 05/09/2007 baada ya wanachama waliokua ndani ya vikundi vya VICOBA kuungana na kuanzisha SACCOS

Kwa sasa UVIMA SACCOS LTD inahudumia mtu yeyote hata kama sio mwanakikundi wa VICOBA ili mradi akidhi hitaji la fungamano letu.

Mwaka wa Fedha wa Chama unaanzia Januari 01 hadi Desemba 31 ya kila mwaka husika

Muundo wa Chama

UVIMA SACCOS LTD

Muundo wa Chama UVIMA SACCOS LTD ☆

MWANACHAMA

Mwanachama mwenye hisa kamili ndiye mmiliki halali wa SACCOS na ndiye anayeendesha Chama (Kupitia Mikutano Mkuu)

Pia Mwanachama ana haki ya kushiriki katika Uongozi (Kuchagua au kuchaguliwa)

BODI YA CHAMA

Mungubariki J. Tarimo MWENYEKITI WA BODI

Wajibu wa Bodi

Kwa mujibu wa Sheria Bodi ya Uongozi wa Chama inatakiwa kuwa na wajumbe wasiopungua watano (5) na wasiozidi tisa (9) akiwemo mwenyekiti na makamu wake.

Wajibu wa Bodi ni kusimamia shughuli zote za utendaji wa chama ikiwemo;

  1. Kuajiri na kuteua watumishi wenye sifa za kutosha kutenda shughuli za Chama wakiwemo Meneja, Mhasibu, Mweka Hazina au watumishi wengine ambao wataendesha shughuli za kila siku za chama

  2. Kuingia mikataba mbalimbali kwa niaba ya chama kwa kuzingatia Kanuni za Vyama vya Ushirika;

Msemaji wa Bodi/Chama:

Mwenyekiti ndiye msemaji mkuu wa chama.

WAJUMBE WENGINE WA BODI

  • Samwel Ch. Mosha

    Makamu Mwenyekiti

  • Mthiolojia Cuthbert N. Moshi

    Mjumbe

  • Safinaeli M. Tarimo

    Mjumbe

  • Jackson S. Shayo

    Mjumbe

KAMATI YA USIMAMIZI

Wajibu wake ni kukagua shughuli za SACCOS na kujiridhisha kuwa SACCOS inaendeshwa kwa mujibu wa sheria, masharti, sera na maazimio mbalimbali ya Mikutano Mikuu

WAJUMBE WA KAMATI YA USIMAMIZI

  • Eldavis Salvatory Elihuruma

    Mwenyekiti

  • Rogathe Robert Minja

    Katibu

  • Rogathe August Minja

    Mjumbe

WAFANYAKAZI

  • JACKSON MTUI

    Meneja

  • GODLISTEN M. SHAO

    Mhasibu

  • Hosiana G. Urio

    Karani

  • Jackline E. Mshanga

    Afisa Mikopo

  • JACKLINE S. MWANGA

    Afisa Mikopo

  • EMANUEL MOTTEY

    Afisa Masoko