UVIMA SACCOS LTD

REG. PRI-KJR-MSH-DC-2022-1427

LICENCE. MSP3-TCDC-2023-00333

KARIBUNI

Mwanachama Bora 2024 akipokea Cheti cha Pongezi na Zawadi toka kwa Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa 17 uliofanyika 20/11/2024

MAZINGIRA NI UHAI

Tuyatunze, Tuyalinde ili Tuishi

UVIMA ni taasisi ya Kifedha (SACCOS) iliyoanzishwa mwaka 2007

Chama hiki cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) kinachohudumia Watu Binafsi na Vikundi, kilichoanzishwa baada ya … soma zaidi

Jumatatu - Ijumaa

Kuanzia 2:30 asubuhi - 10:00 jioni

Jumamosi, Jumapili na Sikukuu ni Mapumziko … soma zaidi

Biashara kubwa ya Chama ni Mikopo

Mikopo hii hutolewa kwa wanachama pekee, ikiwemo Vikundi wanachama baada ya kutimiza masharti ya Mkopo

Chama hutoa Mikopo kama ifuatavyo;

  1. Mkopo wa Dharura

    Mkopo huu ni kwa mwezi 1 tu

  2. Mikopo ya kijamii na uzalishaji

    Mikopo hii ni ya muda mrefu, mwaka 1 hadi miaka 2

    Soma zaidi kuhusu sifa na vigezo vya kupata mkopo hapa …

Mdau ni Mtu au taasisi yeyote ambayo kwa namna moja amba nyingine anafaidika kutokana na shughuli na huduma za Chama

Mwanachama wa UVIMA ndiye Mdau Mkuu na MMILIKI wa SACCOS

Wadau wengine ni;

  1. Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC)

  2. Benki na Taasisi za Kifedha

  3. Taasisi Miamvuli

  4. Wasambazaji (Watoa Huduma)

    Soma zaidi kuhusu wadau wetu hapa…

Baadhi ya huduma Nyinginezo ni;

  1. Uhamasishaji na Ukusanywaji wa Hisa, Akiba na Amana

  2. Elimu juu ya Utunzaji wa Mazingira

  3. Uhamasishaji na Usimamizi wa Vikundi Biashara na VICOBA

  4. Elimu na Mafunzo juu ya Kilimo Hai

    soma zaidi

MADHUMUNI YA UVIMA SACCOS

Kuondoa umaskini na kukuza kipato kwa kuinua, kuimarisha na kuendeleza hali ya kiuchumi na kijamii ya wanachama wake kwa kufuata Sheria, Kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika.

Aidha, Shughuli za msingi kwa UVIMA ni kuhimiza uwekaji wa fedha ambao ni akiba (savings) na upatikanaji wa mikopo kwa wanachama na wazalishaji wadogo.

Eneo la Shughuli za UVIMA SACCOS

Ni Tanzania Bara hususani katika Mkoa wa Kilimanjaro, ndani ya Wilaya ya Moshi

 

UJUMBE MAALUMU TOKA KWA MENEJA

Tuamshukuru sana Mungu kwa kutuwezesha Kufanya Mkutano Mkuu wa 17 tarehe 20 Nov. 2024. Mkutano huu uliambatana na Uzinduzi wa Tovuti hii pamoja na Mobile App.

Mgeni Rasmi katika Mkutano huu alikuma Mama Edith Banzi ambaye ni mwanzilishi wa SACCOS hii (wakati akiwa Mkurugenzi wa Shirika la Floresta Tz 2004 - 2011)

Pia kupitia Mkutano huu, Chama kilitoa Cheti cha Pongezi na zawadi kwa Mwakachama Bora wa SACCOS... Soma zaidi kuhusu Mkutano Mkuu wa 17 wa UVIMA

TULIPOTOKA

Hapo awali SACCOS hii ilikuwa ikihudumia wanachama waliounganishwa kupitia vikundi vya Kijasiriamali ikiwemo VICOBA. Kutokana na mtaji wa Chama kukua, pamoja na mahitaji makubwa ya huduma za kifedha katika jamii inayotuzunguka, Chama kilifikia wakati wa kufanya mabadiliko ya Kisera, Masharti na miongozo mbalimbali ili kupanua wigo na fungamano letu na hatimaye kuweza kuhudumia wanachama nje ya vikundi. Hivyo kwa sasa UVIMA SACCOS inapokea na kuhudumia mtu yeyote atakayekidhi vigezo vya fungamano letu.

Kwa undani zaidi juu ya SACCOS hii, tafadhali nakukaribishwa kwa moyo wa ukunjufu kutembelea tovuti hii kwani utaweza kupata uelewa zaidi juu ya... Soma Zaidi

HATI ZA UTAMBULISHO

UVIMA SACCOS LTD

SACCOS ya Kijamii      -           Daraja A

Nambari ya Usajili

Usajili wa zamani - Na. KLR 712

Usajili mpya - Na. PRI-KJR-MSH-DC-2022-1427 

Nambari ya Leseni 

Leseni ya Zamani - Na. MSP3-TCDC-2021-00304

Leseni Mpya - Na. MSP3-TCDC-2023-00333

TRA TIN Na. - 142-184-079

Fungua Akaunti Sasa Ujishindie Zawadi

Unahitaji Msaada?