Twenzetu UVIMA SACCOS

KUMENOGAAA

UVIMA ni nini?

UVIMA ni kifupi cha maneno (Umoja wa Vikundi Marangu)

Hiki ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo kilichoanzishwa na kusajiliwa tarehe 05/09/2007. Chama hiki kilipewa namba ya usajili KLR 712 chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya 2003

Mnamo mwaka 2022 UVIMA SACCOS ilipata usajili mpya Na. PRI-KJR-MSH-DC-2022- 1427

Aidha, mnamo tarehe 04/07/2023 UVIMA ilipata Leseni mpya ya kutolea huduma ndogo za kifedha; Leseni Na. MSP3-TCDC-2023-0033. Leseni hii ilitolewa chini ya kifungu cha 20 cha Sheria ya Huduma Ndogo za Kifedha Na. 10 ya  mwaka 2018 baada ya Chama kutimiza matakwa yote ya Kisheria.

KWA NINI UVIMA ILIANZA KAMA UMOJA WA VIKUNDI?

Chama hiki kilianzishwa baada ya vikundi vya VICOBA vilivyokuwa chini ya uangalizi wa Shirika lisilo la kiserikali “Floresta-Tanzania” ambalo ndio waasisi wa VICOBA katika Mkoa wa Kilimanjaro, kuona kuwa kuna haja ya kuanzisha chombo cha umoja ili kutoa nafasi nzuri kwa wanachama wake kukopa mikopo mikubwa zaidi na kwa riba nafuu zaidi.